Serebuka (Cheza na Mwalimu) kama neno lenyewe linavyosema ni sanaa ambayo ipo kwenye mfumo wa muziki, ngoma kwa ajili ya kuburudisha na kufurahisha watazamaji wa luninga.
Serebuka (Cheza na Mwalimu) ina lengo la kutafuta vipaji vya watu ambao ni maarufu kwenye jamii yetu ambao fani zao walizopatia umaarufu si katika kusakata dansi au ngoma bila kuangalia rangi zao au umri.
Wanashindana kwa kucheza kila wiki kwa jozi(pair) baada ya kupatiwa mafunzo ya muziki watakaocheza siku ya kurekodi kipindi. Na watazamaji wanapata nafasi ya kuwapigia kura kwa njia ya SMS ya nani wanayemtaka abakie halafu mwenye kura chache anatoka.
Saturday, May 1, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Aisee mbona sielewi kuhusu hii Serebuka, yupo waki Masoud Masoud, Jini Kabula na Yusufu Mlela? Wemebadilishwa na hata taarifa zao hazipo.
ReplyDeleteSidhani kama hili ni swala zuri sana hususani ni kwa sisi watazamaji ambao tunapenda kuwaona watu hawa.
wachezaji wote wanajitahidi vya kutosha,lakini muda munaotuonyesha ni mdogo,kuna baadhi ya makundi wanapata muda wa kutosha lakini makundi mengine muda unakua mdogo sana
ReplyDeleteyote tisa kumi group namba kumi(10) wanatisha na mpaka sasa
wanaongoza kwa kila kitu .kiufupi wako juu
haya hapa kwenye kuvote kundi gani unataka lishende kundi No. 5 mbona silioni au watolewa kiaina, tunaomba kujua tatizo ni nini
ReplyDeleteMuda jamani serebuka inatuburudisha, ila kama alivyosema burej, kuna makundi baadhi tumeshanote yanapewa muda mchache na wengine wanapewa muda mrefu Why!!!!!!!!!!! tunaomba kuhoji, au mshindi anajulikana!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteUShauri wa chee kabla ya kuadvertise haka kablog kwenu mngeweka details zakutosha! mmenipotezea muda wandu kwani nuilitegemea nikute mengi zaidi ya yale nayokutana nayo luningani
ReplyDelete